Na Mwandishi wetu Moshi, Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga, amekutana na kundi la watu wenye ulemavu katika ziara iliyowakutanisha na wanufaika wa mikopo ya 10% ya mapato ya Halmashauri (2% kwa wenye Ulemavu) na wale ambao wameomba na hawajapata.
Ziara hiyo imelenga kujadili maslahi,fursa na changamoto mbalimbali za watu wenye ulemavu imefanyika leo tarehe 28 Februari 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Halmashauri Wilaya ya Moshi.
"Ninamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo kwa kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye ulemavu na ninawahimiza watu wenye ulemavu kuchangamkia Fursa hizo na kujitokeza katika kupata zabuni za tenda za serikali kwa mfumo wa manunuzi ya umma (30% kwa watu wenye ulemavu) zinazotolewa ili kuwaletea tija na kujikwamua kiuchumi" amesema hayo Naibu Waziri Mhe. Nderiananga.

Pia, ameutaka Uongozi wa Wilaya ya Moshi kuhakikisha unaeaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwapa Fursa za Tenda za manunuzi ya ndani kwa makampuni ya vikundi vya watu wenye ulemavu ili kuwasaidia watu wenye ulemavu kuondoka kwenye umaskini.
Aidha, amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Moshi na Uongozi wote kwa kukata kiu ya Mheshimiwaa Rais ya kuwasikiliza wananchi na kuwaletea faraja Watanzania kwa kutoa mikopo ya Asilimia 2% kwa kiwango cha 98% yaani shilingi 60.4M, pia hata wale ambao bado hawajanufaika wameondoka hapa wakiwa na Matumaini.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Godfrey Mzava ameihakikishia jamii ya watu wenye ulemavu kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuwasaidia na kuwakwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa, Serikali iko tayari kushirikiana na Jamii na Vyama vyote vya watu wenye ulemavu na itatetenga eneo maalumu la biashara kwaajili ya watu wenye ulemavu ili wafanye biashara zao vizuri.
Naye, Bw. Mwacha, Mlemavu wa viungo na mnufaika wa Mkopo aliyemaliza deni lake amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwapa vipaumbe na kuahihidi kuendelea kuhamasishana na kuelimishana kuhusu umuhimu wa mikopo hii ili kutoka kwenye dhana ya utegemezi.







Social Plugin