Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIRECU YAANDIKA HISTORIA MPYA YA USHIRIKA, MKUTANO MKUU WAPITISHA BAJETI ZAIDI YA SH BILIONI 2.8

 

Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga Ibrahim Kakozi akizungumza kwenye mkutano mkuu wa SHIRECU

Meneja  wa Chama cha Ushirika SHIRECU Alphonce Makasi  akisoma  rasimu  ya  bajeti  kwenye mkutano Mkuu wa 31 

                   Chama Kikuu Cha Ushirika Mkoani Shinyanga (SHIRECU)  kimepitisha rasimu ya  bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 2.8  kwa mwaka wa fedha 2026/2027 huku ikijizatiti kuanza  kukopesheka  kwenye taasisi za kifedha.

Bajeti hiyo limepitishwa leo  April 28, 2026   baada ya Meneja  wa chama cha ushirika Shirecu Alphonce Makasi  kuwasomea  taarifa na rasimu  ya  bajeti  kwenye mkutano Mkuu wa 31  uliowakutanisha  wajumbe  202 kati ya wajumbe 214  waliokuwa wakitakiwa kuhudhuria kwenye mkutano huo.

Akisoma taarifa hiyo Meneja Makasi amesema wajumbe wakiridhia kupitishwa kwa bajeti zaidi ya shilingi bilioni 2.8  na kukopa kwenye taasisi za kifedha wataweza kutimiza adhima ya mipango ya kuendeleza biashara ya ununuzi wa mazao.

Pia mazao hayo yatakuwa Mchanganyiko,uanzishwaji na kufufua kiwanda kipya cha kukamua mafuta ya alizeti na kuendeleza duka la pembejeo.

“Awali taasisi za kifedha zilikataa kabisa kutukopesha kutokana na kuwepo kwa vikwazo vya deni kutoka benki ya Uwekezaji ya (TIB) lakini sasa tumeanza kuonyesha uaminifu wa kulipa na kupata ruhusa ya kuendelea kukopesheka kwenye taasisi za kifedha zozote nchini”amesema Makasi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Shirecu Naomi Chaba amesema  kuna vyama vya ushirika (Amco’s) 107 na wanachama 7413, ambapo mpango ulioanza mwaka 2025 hadi  Februari  2026  wamefanikiwa kununua mazao Mchanganyiko kama choroko na dengu,kugawa kompyuta mpakato 50 nakutoa mafunzo

"Pia ,tumefanikiwa kukarabati shule ya sekondari Buluba  na kusomesha wanafunzi 28  wa kidato cha tano kwa awamu,  kwa gharama ya shilingi Milioni 45."    pia  Chama kinatarajia kujenga kiwanda cha dengu kufanya biashara ya pamba ukarabati wa magala ,  amesema Chaba

Naye  Mrajis msaidizi  wa Ushirika mkoa wa Shinyanga Ibrahim  Kakozi amesema taasisi za kifedha   sasa zikae sawa kuwakopesha shirecu  huku akiwataka wajumbe waeleze yale ambayo wanataka yatekelezwe na yakikwama waihoji bodi  nakutoa ushauri zaidi nini kifanyike ili kuboresha zaidi.

"Niombe kila Amcos iripoti kila tatizo lililopo ili chama kiweze kufuatilia na kujua tatizo nini, kwani mkileta kwa barua itakuwa ni rahisi kufuatiliwa kwa haraka zaidi"amesema Kakozi.

        Mwakilishi wa COASCO Rodrick Kilemile 
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga akizungumza kwenye mkutano wa SHIRECU

Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga Ibrahim Kakozi akizungumza kwenye mkutano mkuu wa SHIRECU
Wajumbe wa mkutano wa SHIRECU

Mkutano unaendelea

Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga Ibrahim Kakozi akizungumza kwenye mkutano mkuu wa SHIRECU




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com