Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZWA KULIOMBEA TAIFA NA KULINDA AMANI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakati wa hafla ya kusimikwa Uongozi waKitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.

************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Viongozi wa Dini wana wajibu wa pekee wa kuliombea Taifa kama ambavyo Biblia Takatifu ilivyoelekeza.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa wa hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.

Amewahimiza kuendelea kumuombea afya njema,busara na hekima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ndiye kiongozi Mkuu wa Nchi na kupitia yeye nchi itaendelea kuwa salama. 

Amewataka Viongozi hao kutambua wanapaswa kutimiza wajibu na kuwa na moyo wa utumishi kwa nchi, waumini na Kanisa kwa ujumla.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amewahimiza Viongozi wa Dini kutambua wajibu wa kulinda mazingira kwa kuendeleza jitihada za uhifadhi mazingira na kuwafundisha waumini kujiepusha na ukataji miti, uchomaji misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji.

 Aidha amewasihi kutoa mafundisho yatakayoichagiza upandaji miti mipya kwa wingi kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amesema pamoja na utoaji wa eneo la hekari 12 mkoani Dodoma kwaajili ya ujenzi wa makao makuu ya Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), pia Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 100 kwaajili ya kuanzisha ujenzi huo.

Amesema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliunda Wizara maalum kusimamia mahusiano ambayo imeendeleza ushirikiano baina ya Serikali na Taasisi za dini. 

Ameshukuru Taasisi za dini kwa mchango wanaotoa katika huduma za kijamii kama vile shule na huduma za Afya pamoja na malezi ya watoto.

Amewaomba Viongozi hao wa dini kusimamia maadili ya nchi kwa kujenga Taifa la watu wanaoheshimu na wanaojali uwepo wa Mungu. Vilevile kujenga Taifa la watu waaminifu, wanaoheshimiana, wanaopenda nchi, kushirikiana na kuepusha Taifa la watu wabinafsi na wapenda rushwa. 

Aidha, Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kusimamia amani ya nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu amesema wamefanikiwa kufanya utambuzi na kuendelea kuwafikia makundi yote ya Mahusiano yakiwemo Taasisi za Dini, Asasi za Kiraia, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Vyama vya Wafanyakazi, Chama cha Waajiri, Kamati za Amani na Maridhiano na Vyama vya Siasa.

Amesema kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma tumefanikiwa kupata eneo la CPCT kuweza kujenga Makao Makuu yao katika Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma.

"Walileta ombi lao la kutafutiwa eneo la ukubwa wa ekari 10, Serikali imefanikiwa kupata eneo la ekari 12 pale Mtaa wa Ipala, karibu na Mji wa Serikali Mtumba na tumewajulisha uongozi wa CPCT kuhusu hilo kwa hatua ya kuendelea na taratibu za kukamilisha umiliki". Amesema
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakati wa hafla ya kusimikwa Uongozi waKitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akizungumza wakati wa hafla ya kusimikwa Uongozi waKitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishuhudia kuapishwa kwa Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), Askofu Dkt. Vernon Fernandes, wakati wa hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano waBaraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katikaUkumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leotarehe 06 Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiungana na Viongozi mbalimbali wa Makanisa yaKipentekoste Tanzania, katika kufanya maombi maalum ya kumuombea Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Taifa kwa ujumla wakati wa hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifawa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, JijiniDar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com