Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UPENDO NA MAELEWANO VYATAJWA KUWA MSINGI WA AMANI NCHINI



Na mwandishi wetu,Dar

Adam Seleman, Mkazi wa Msongora Jijini Dar Es Salaam amesema tafsiri halisi ya amani ni pamoja na kuelewana na kupendana miongoni mwa Watanzania, akihimiza upendo na maelewano kama msingi wa kudumisha amani na utulivu nchini.

Bw. Selemani amebainisha hayo leo Jumamosi Februari 07, 2026 wakati akizungumza na mwandishi wetu wa habari kuhusu umuhimu wa amani kwa ustawi na maendeleo, akisema familia, Jamii na Nchi yoyote inahitaji amani na utulivu ili kuweza kutimiza majukumu na wajibu walionao.

"Maana halisi ya amani ni ile hali ya mtu kuwa na uhuru wa kufanya jambo ambalo linaruhusiwa Kikatiba na pia amani tafsiri yake ni upendo, tukipendana ndio amani yenyewe kuanzia ndani ya nyumba. Nawaomba sana tuendelee kushikamana na kudumisha hiki tulichonacho kwani sisi nchi yetu ni kisiwa cha amani." Amesema Bw. Selemani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com