Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TEAM FEBRUARY WASHEREHEKEA SIKU ZA KUZALIWA 'BIRTHDAY' NA WAZEE KOLANDOTO SHINYANGA


Kikundi cha watu maarufu kama Team February, kinachojivunia wanachama waliozaliwa mwezi Februari, kimeonesha mfano bora wa upendo na mshikamano kwa jamii kwa kufanya matendo ya huruma kwa wazee na wasiojiweza wanaoishi katika Kituo cha Kolandoto, Manispaa ya Shinyanga.

Wanachama wa Team February mkoani Shinyanga leo Februari 27, 2026, wameadhimisha siku zao za kuzaliwa kwa namna ya kipekee kwa kuamua kugusa maisha ya wahitaji badala ya kusherehekea peke yao.

Katika hafla hiyo ya kijamii, wamekabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wazee waliopo kituoni hapo, ikiwa ni pamoja na mahitaji muhimu ya kila siku.

Mbali na kukabidhi misaada hiyo, wanachama hao wameshiriki kwa pamoja na wazee hao kukata keki kama ishara ya kusherehekea maisha na kuimarisha upendo baina yao.

Tukio hilo limejaa furaha na hisia za kuguswa, huku wazee wakionekana kufurahia kushirikishwa katika sherehe hiyo maalum.Kwa kufanya hivyo, Team February wameweka mfano kwamba sherehe za kuzaliwa zinaweza kuwa fursa ya kurudisha kwa jamii, kuimarisha mshikamano na kuleta tabasamu kwa wale wanaohitaji zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com