
Hisia hizi zinaungwa mkono kwa dhati na Victoria Mkwizu kutoka Iringa, anayekumbusha kuwa vurugu hazichagui, na waathirika wakuu mara zote ni wanawake na watoto. Kilio chake ni cha kuitaka jamii idumishe utulivu ili kila familia iweze kuishi bila wasiwasi.
Amani inapotoweka, si tu maendeleo yanashama, bali hata udugu na mshikamano wetu kama Watanzania unaharibika. Hivyo, kila sala na dua inayopandishwa na kila mmoja kwa imani yake iwe ni kwa ajili ya kuilinda Tanzania dhidi ya chuki na machafuko.
Wito huu unahitimishwa kwa busara na Nuhu Ally kutoka Morogoro, akiwaelekea vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa. Amewasihi vijana kuitumia teknolojia na mitandao ya kijamii kama daraja la kujikwamua kiuchumi na si kama silaha ya uchochezi.
Uzalendo wa kweli kwa kijana wa sasa ni kuilinda amani iliyopo ili iweze kumpatia fursa ya kujenga maisha yake na ya taifa lake. Kwa umoja huu, na kwa kila mmoja kusimama kwenye nafasi yake kwa imani na matendo, Tanzania itazidi kubaki kuwa nchi ya mfano, yenye amani inayotiririka kama mto usio kauka.
Social Plugin