Msanii wa nyimbo za asili nchini Tanzania, Elizabeth Maliganya maarufu kama Omkaya Eliza, ameachia rasmi wimbo wake mpya unaoitwa “Bhalemi (Wakulima)”, wimbo unaobeba ujumbe mzito wa kuwatambua, kuwahimiza na kuwaenzi wakulima kama mhimili wa uchumi na maisha ya jamii.
Kupitia sauti yake ya kipekee na ala za asili, Omkaya Eliza amefanikisha kuwasilisha ujumbe unaogusa maisha ya wakulima.
“Bhalemi (Wakulima)” ni wimbo unaoendana na uhalisia wa maisha ya Watanzania wengi, hususan wale wanaojihusisha na kilimo, huku ukiwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taifa.
Video ya wimbo huo imejaa taswira halisi za maisha ya wakulima na shughuli za kilimo, jambo linalozidi kuupa uzito na uhalisia ujumbe unaowasilishwa.
🎥 Tazama video ya wimbo “Bhalemi (Wakulima)” hapa:
👉 https://youtu.be/QtrGgWa_MJw?list=RDQtrGgWa_MJw

Social Plugin