Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHEREHANI AITAKA TARURA KUIMARISHA USIMAMIZI WA WAKANDARASI, ASISITIZA UBORA NA USALAMA WA BARABARA


Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, ameshauri Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuimarisha usimamizi wa wakandarasi wanaopewa miradi ya ujenzi na matengenezo ya barabara ili kuhakikisha wanazingatia viwango vya ubora na usalama wa wananchi.

Cherehani ametoa rai hiyo Februari 24, 2026, wakati akichangia hoja kwenye Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Amesema baadhi ya wakandarasi wamekuwa wakichimba mashimo kando ya barabara bila kuchukua tahadhari stahiki, hali inayohatarisha usalama wa vyombo vya usafiri na wananchi wanaotumia barabara hizo.

Aidha, ameomba kurejeshwa kwa mfumo wa awali ambapo kila Halmashauri ilikuwa na Meneja wake wa TARURA, akieleza kuwa hatua hiyo itaongeza ufanisi na uwajibikaji katika usimamizi wa miradi ya barabara inayotekelezwa katika maeneo husika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com