
Siasa hizo za kichochezi zimebuma, kwani lengo lao la kukwamisha miradi ya kimkakati inayolenga kumkomboa mwananchi wa kawaida, kwa kuziauhalisia wa ushirikiano wa kimataifa unazidi kuonyesha kuwa dunia ina imani kubwa na mwelekeo wa sasa wa nchi katika kuimarisha utawala bora na uchumi wa watu.
Katika kielelezo cha hivi karibuni cha imani hiyo, Tanzania na Benki ya Dunia zimefanya mazungumzo yenye tija jijini Berlin, Ujerumani, mnamo Januari 16, 2026, yaliyolenga kuimarisha sekta ya kilimo kupitia Mpango wa Uhimilivu wa Mfumo wa Chakula (TFSRP) na mpango mpya wa AgriConnect.
Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Daniel Chongolo, alikutana na Kaimu Mkurugenzi wa Kimataifa wa Benki ya Dunia, Bi. Marianne Grosclaude, pembeni mwa Jukwaa la 18 la Kimataifa la Chakula na Kilimo (GFFA) na kujadiliana namna ya kuongeza tija katika kilimo cha wakulima wadogo. Hatua hii ya Benki ya Dunia kuendelea kumwaga mabilioni ya fedha, ikiwemo dola milioni 300 kwa ajili ya kuimarisha mifumo endelevu ya chakula na upimaji wa afya ya udongo, ni kielelezo kuwa kelele za uzushi mitandaoni hazina nafasi mbele ya takwimu na mipango thabiti ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Aidha, katika mazungumzo hayo, Tanzania imewasilisha maombi ya kupata msaada zaidi katika maeneo ya kilimo kwa kutumia mashine za kisasa, ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhia mazao ili kupunguza upotevu baada ya kuvuna, na upanuzi wa mifumo ya umwagiliaji nchi nzima.
Benki ya Dunia imekubaliana na mapendekezo hayo ikisisitiza kuwa Tanzania ni nchi muhimu ya majaribio katika utekelezaji wa programu zenye matokeo makubwa kwa jamii.
Kushindwa kwa ajenda za wanaharakati wanaojaribu kuzuia misaada na mikopo hii ni ushindi kwa wakulima wa Kitanzania ambao sasa wanakwenda kunufaika na kilimo cha kibiashara kitakachowaletea tija, usalama wa chakula, na chachu ya ukuaji wa uchumi wa Taifa, kinyume na matamanio ya wale wanaotaka kuona nchi ikikwama.
Kufuatia hali hiyo, Watanzania wametakiwa kuwa makini na taarifa wanazokutana nazo mitandaoni na kupuuza madai yanayosambazwa na watu wenye nia zisizo njema ambao hupata faida kwa kuona nchi ikiingia katika taharuki au kutengwa.
Serikali imesisitiza kuwa itasimama kidete kukemea hali hiyo huku ikijielekeza katika kufanya kazi zenye kuonekana, kama vile mwaliko wa kimkakati ambao Tanzania imepewa na Benki ya Dunia kushiriki katika Mpango wa Athari za Maarifa utakaofanyika nchini Zambia mwishoni mwa Februari 2026. Huu ni ushahidi mwingine kuwa siasa za majitaka na uzushi zimepitwa na wakati, na badala yake diplomasia ya kiuchumi na maendeleo ya kweli ndiyo yanayoshika hatamu katika kuijenga Tanzania mpya.
Social Plugin