Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI WA CHADEMA MBEYA WASHIKILIWA WAKIHAMASISHA MIKUSANYIKO BATILI




Na mwandishi wetu, Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Mbeya Bw. Masaga Pius Kaloli na Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Mbeya Elisha Chonya kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya mikusanyiko isiyokuwa halali.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema watuhumiwa hao walikamatwa Januari 21, 2026 saa tisa alasiri katika Kijiji na Kata ya Inyala baada ya Polisi kupata taarifa za uwepo wa Viongozi hao katika eneo hilo wakifanya maandalizi na wakiwahamasisha watu kukusanyika ili kufanya Mkutano bila bila kufuata taratibu za kisheria zilizopo.

"Pamoja na kukiuka kwa makusudi taratibu hizo za kisheria, ikimbukwe kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimezuiliwa na Mahakama kufanya shughuli zozote za kisiasa." Amesema Kamanda Kuzaga.

Taarifa hiyo ya Polisi Mkoa wa Mbeya imeendelea kueleza kuwa upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com