Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKAMBA AZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI UMEME NGAZI YA VITONGOJI KAHAMA



Na Marco Maduhu, KAHAMA

NAIBU Waziri wa Nishati na Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, amezindua mradi wa usambazaji wa umeme ngazi ya vitongoji Manispaa ya Kahama.

Amezindua mradi huo leo Januari 10,2026 katika kitongoji cha Majengo na Chapulwa Manispaa ya Kahama, kwa kuwasha umeme kwenye nyumba za watu binafsi, na taasisi za Serikali katika Zahanati ya Chapulwa.

Makamba akizungumza kwenye hafla hiyo, amesema kazi waliyopewa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Wizara ya Nishati, ni kuwasha umeme tu.


" Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ametuagiza tufanye kazi ya kuwasha umeme, na hapa Kahama ametupatia maelekezo, kwamba ifikapo mwezi Julai, vitongoji vyote vya Kahama tuwe tumeshawasha umeme, " amesema Makamba.

Amesema, Rais ameagiza pia kwa wananchi ambao watashindwa kufunga mifumo ya umeme kwenye nyumba zao, na wenyewe wafanyiwe namna ya kuwekewa umeme, na kwamba maelekezo yake hadi ifikapo 2030 Kaya zote ziwe umeme.


"nimerudi nyumbani na habari njema ya kuwasha umeme, mimi ni kazi tu,nataka Watanzania wakisikia jina la Salome Makamba wajue tuna washa umeme," ameongeza Makamba.

Amesema nchi ya Tanzania haina changamoto ya umeme, sababu umeme upo wa kutosha na wauhakika, na kwamba umeme ni kichocheo kikubwa cha uchumi.


Amewataka pia wananchi, waitunze miundombinu ya umeme, na kuacha kuiba vifaa vya miundombinu hiyo, huku akiwaomba Jeshi la Jadi Sungusungu kusaidia kupambana na uhalifu huo.

Aidha, ametoa wito pia Watanzania kwamba waachane na matumizi ya nishati chafu ya kupikia, bali watumie majiko banifu na gesi, na kwamba serikali itakuja na mpango kabambe wa kuweka ruzuku kwenye majiko hayo, ili wananchi wanunue kwa bei ndogo.


Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Benjamini Ngayiwa, ameshukuru kwa uzinduzi wa mradi huo, na kwamba katika Manispaa hiyo kuna vijiji 42 na vyote vina huduma ya umeme, na kwamba kati ya vitongoji 218, vitongoji 83 vina umeme, huku 135 bado havina umeme na kushukuru kwa uzinduzi wa mradi huo.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati vijijini (REA) Mhandisi Jones Olotu, amesema katika Mkoa wa Shinyanga kuna vitongoji 2,704 na vitongoji 1,205 tayari vina umeme, na 1,496 bado, na tarehe 17 wanakwenda kusaini mikataba ya kusambaza umeme ngazi ya vitongoji.


Amesema, katika Manispaa ya Kahama wanakwenda kuwasha umeme kwenye vitongoji 581, ambapo uzinduzi wake umezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba, na kwamba katika wilaya nzima ya Kahama kuna vitongoji 295.


Nao baadhi ya wananchi waliowashiwa umeme akiwamo Mariam Manyesha, wamesema wamefurahi kuwashiwa umeme, ambao utakuwa kichocheo kikubwa cha ukuzaji wa uchumi.


TAZAMA PICHA👇👇

Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akizungumza.

Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akizungumza.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama Glory Absalum akizungumza.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati vijijini (REA) Mhandisi Jones Olotu.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Benjamini Ngayiwa akizungumza.

Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akiwasha umeme kwenye nyumba ya Bwana Kulwa Malale mkazi wa kitongoji cha Majengo Kata ya Wendele Manspaa ya Kahama.

Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akibonyeza alam kwa ajili ya kuzindua Rasmi mradi wa usambazaji umeme ngazi ya vitongoji Kahama.


























Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com