Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TABORA WAUPOKEA MWAKA MPYA KWA AMANI NA UTULIVU MKUBWA



Wananchi wa maeneo mbalimbali Mkoani Tabora wameshiriki kwa namna mbalimbali kusherehekea sikukuu ya Mwaka mpya 2026 na kuuaga mwaka 2025, Burudani za muziki katika sehemu mbalimbali za starehe zikionekana kujaa zaidi, amani na utulivu ukitawala pia katika maeneo hayo.

Wengine pia kama ilivyo utamaduni wa wananchi wa Tabora, wameonekana jana usiku Januari Mosi, 2026 wakiwa kwenye mitaa mbalimbali wakiimba na kusherehekea kuumaliza mwaka 2025 na kuuanza mwaka mpya 2026.

Polisi pia wameonekana katika maeneo yote yenye mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inakuwepo ili kutoa fursa ya kila mmoja kufurahi na wengine kuendelea na biashara zao bila ya vitisho vyovyote vya uvunjifu wa amani kwenye jamii.

Jana Disemba 31, 2025 wakati wa hotuba yake ya kuukaribisha mwaka Mpya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, aliwatakia kheri na mafanikio tele watanzania wote, akiahidi kwamba serikali yake itaendelea kuwatumikia watanzania wote kikamilifu ikiwa ni pamoja na kujenga umoja wa Kitaifa nchini, akitoa rai ya kutokubali kugawanyika kiitikadi na kimtazamo wanapoendelea na ujenzi wa Taifa lao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com