
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (katikati) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia Professa Maulilio Kipanyula,(kulia) akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Bweno katika taasisi hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike yenye jumla ya vyumba 184 katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
.....
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeeleza kuridhishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), kufuatia ziara ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, iliyofanyika jana katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri alikagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike yenye jumla ya vyumba 184, mradi unaolenga kuongeza ushiriki wa wanawake na watu wenye ulemavu katika elimu ya juu, hususan katika fani za sayansi, teknolojia na ubunifu ambazo ni nguzo muhimu katika maendeleo ya taifa.
Aidha, Mhe. Wanu alipokea taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Samia Scholarship Extended (DS/AI+), unaodhamini wanafunzi 50 wanaosoma fani za Sayansi ya Takwimu, Akili unde (Artificial Intelligence—AI) na Sayansi Shirikishi. Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuandaa rasilimali watu wenye ujuzi wa kisasa unaokidhi mahitaji ya soko la ajira sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mhe. Naibu Waziri aliipongeza NM-AIST kwa usimamizi mzuri na hatua iliyofikiwa katika kutekeleza miradi hiyo, akisisitiza kuwa miradi hiyo ni muhimu katika kuimarisha elimu ya juu, kukuza utafiti na kuandaa wataalamu watakaoharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia Professa Maulilio Kipanyula, alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa mabweni imefikia asilimia 80 na inatarajiwa kukamilika Februari 2026.
Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuishi kwa wanafunzi wa kike na kuongeza motisha kwao kushiriki kikamilifu katika masomo ya sayansi na teknolojia.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (katikati) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia Professa Maulilio Kipanyula,(kulia) akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Bweno katika taasisi hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike yenye jumla ya vyumba 184 katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir,akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike yenye jumla ya vyumba 184 katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia Professa Maulilio Kipanyula,akizungumza mara baada ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir kufanya ziara katika taasisi hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike yenye jumla ya vyumba 184 katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.

Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (hayupo pichani),akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike yenye jumla ya vyumba 184 katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha. 

Social Plugin