Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KANISA LA ACK WAIRIMA LASHAMBULIWA KWA MABOMU, GACHAGUA ANUSURIKA



Makabiliano makubwa yameshuhudiwa katika Kanisa la ACK Wairima, Kaunti ya Nyeri alikokuwa anahudhuria ibada ya leo Jumapili Januari 25, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. Rigathi Gagachua.

Kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, Polisi waliokuwa wamefunika nyuso zao wametupa mabomu ya kutoa machozi na kurusha risasi za moto katika kanisa hilo, watu kadhaa wakijeruhiwa huku Gagachua na ujumbe wake wakofanikiwa kutoroka.

Hii si mara ya kwanza kwa Naibu huyo wa Rais wa zamani kushambuliwa kanisani ambapo Wiki mbili zilizopita shambulio kama hilo lilitokea nje ya kanisa la Independent Pentecostal Church of Africa (AIPCA) huko Kiamworia, Gatundu Kusini ambapo mafuriko yalitokea baada ya makundi hasimu ya vijana waliokuwa na virungu kuhusika katika vurugu nje ya Kanisa hilo.

Kwenye chapisho lake kwenye Mtandao wa X Gagachua amedai kuwa yeye na washirika wake walinaswa ndani ya Kanisa hilo baada ya shambulio hilo kutokana na kile alichokiita Jaribio la mauaji, akitoa wito wa wananchi kudumisha maombi dhidi ya amani ya nchi hiyo, akidai pia kuchomwa moto kwa magari yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com