Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 17, 2026 ameongoza kikao cha kazi kuhusu ujenzi wa miradi ya barabara za haraka (Express Ways) kwa ubia kupitia mfumo wa PPP.
Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, kimehudhuriwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile.
Wengine ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. James Kilabuko, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara pamoja na watendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, David Kafulila.




Social Plugin