
Wakati majirani na 'mawakala' wa uongo wakikesha kusambaza propaganda kuwa Bandari ya Dar es Salaam ina kulegalega, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Jemedari Dkt. Samia Suluhu Hassan imewajibu kwa vitendo kwa kuandika historia nyingine ya dhahabu.
Safari hii, si meli ya kawaida, bali ni chuma cha kisasa, Höegh Australis, meli inayotumia nishati safi ya gesi asilia (LNG), imetia nanga katika maji ya Tanzania na "kuelea" kwa mbwembwe ikiwa imesheheni magari 1,006, huku ikithibitisha kuwa Dar es Salaam sasa ndiyo mtembezi wa anga za kimataifa.
Ujio wa meli hii yenye urefu wa meta 200 kutoka kampuni ya Höegh Autoliners (Norway), ni salamu tosha kwa wale waliozoea kudhani Tanzania bado ipo kwenye zama za kale. Huu ni ushahidi kuwa maboresho ya miundombinu si maneno ya majukwaani, bali ni hali halisi inayovutia miamba ya usafirishaji duniani.
Kwa ujio wa meli hii Tanzania imeingia kwenye ramani ya dunia kwa kupokea meli zinazotumia nishati rafiki (LNG), jambo ambalo nchi nyingi jirani bado zinaliota.
“Bandari ya Dar es Salaam sasa ni lango la kimataifa, si la kikanda tu. Maboresho ya miundombinu, matumizi ya teknolojia na huduma za kisasa vimeivutia meli kubwa kama hii,” alisema Prosper Setebe, wakala wa meli hiyo kutoka kampuni ya EACS.
Majibu kwa "Wabishi" na Propagandista
Kwa muda mrefu, kumekuwa na kelele za hapa na pale zikijaribu kupaka matope ufanisi wa bandari yetu. Lakini Höegh Australis imekuja kama "pingu" ya kufunga midomo hiyo. Meli hiyo ilihudumiwa fasta na kuondoka bandarini katika muda zaidi ya sahihi.
"Ufanisi huu kwenye kasi ya kushusha na kupakia mizigo unatokana na mfumo kwenda "ki-digitali".
Aidha meli hii kubwa na nyingine ambazo ni za kimkakati haziwezi kutia nanga kwenye bandari isiyo na usalama na amani ya kudumu, ujio wao ni kudhihirisha kuwa Tanzania ipo tulivu na inaendelea kujenga uchumi wake.
Maboresho haya ni matokeo ya utulivu wa kisiasa na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amefungua milango ya uwekezaji. Wakati wengine wakishangaa meli zinazopita, Tanzania inashangiliwa kwa kuleta meli za kisasa zinazobeba uchumi wa mataifa mengi.
Wakala Setebe ametoa wito kwa wadau wa ndani na nje: "Njooni Dar es Salaam, huku ndipo kwenye ufanisi, huku ndipo kwenye kasi!"
Huku kukiwa na maoni ya hapa na pale mitandaoni, baadhi wakijaribu kupunguza ukubwa wa jambo hili, ukweli unabaki palepale; Tanzania si nchi ya mchezo mchezo. Tumeshawazidi majirani kwa hatua za kiufundi, miundombinu, na uaminifu wa kimataifa.
Kama walitegemea kuona bandari inafungwa, wameambulia kuona meli kubwa zaidi zikiingia. Hii ni Tanzania ya kazi, utulivu, na maendeleo ya kweli.
Social Plugin