Na Mwandishi Maalum, Mwanza
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesisitiza wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kudumisha amani ya Tanzania, akisema amani ndio msingi wa maendeleo na ustawi wa jamii.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 23, 2026 wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa Meli mpya na ya kisasa ya MV New Mwanza, kwenye Bandari ya Kusini, akisema hata maendeleo binafsi ya kila mwananchi yanategemea utulivu na amani.
"Yote tunayoyasema hayawezi kutekelezeka kama hakuna amani, hata shughuli zako wewe mmoja mmoja huwezi kuzitekeleza kama hakuna amani katika eneo lako. Mnufaika namba moja wa amani ni wewe mwenyewe." Amesema Mhe. Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amesisitiza pia umuhimu wa kulinda umoja, utaifa na undugu tuliourithi kutoka kwa watangulizi waliokuwepo, akisema kote duniani amani imekuwa msingi wa mafanikio na ustawi wa wananchi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Social Plugin