Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMANI KWANZA, INTANETI BAADAYE: FUNDISHO LA UGANDA NA MSIMAMO WA TANZANIA

 

Katika mwendelezo wa mazungumzo ya Sherry Party, ujumbe wa Tanzania kwa dunia umekuwa wazi: Amani ni sarafu ya thamani zaidi kuliko teknolojia. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa katika safari ya kuelekea uchumi wa Dola trilioni 1, usalama wa raia hauwezi kuchezewa na "chuki za kidijitali."

Msimamo huu unakuja wakati ambapo nchi jirani ya Uganda na mataifa mengine ya Afrika yameonesha kwa vitendo kuwa, intaneti inapogeuzwa kuwa silaha ya uratibu wa vurugu, serikali zina wajibu wa kisheria na kimaadili kulinda uhai wa watu wake kwanza.

Funzo kutoka Uganda: Amani ni Tunu, si Bidhaa

Nchini Uganda, historia imefundisha kuwa maandamano yanayochochewa na habari za uzushi mtandaoni huishia kwenye uharibifu wa miundombinu na kupoteza maisha ya vijana. Kwa Waganda na sasa kwa Watanzania, fundisho ni moja: Utulivu ndio msingi wa maendeleo. Viongozi wa kanda hii wamebaini kuwa "wachochezi" mara nyingi hujificha maelfu ya maili mbali, wakitumia intaneti kuitumbukiza nchi kwenye giza, huku raia wa kawaida na mama ntilie wakibaki kuteseka mitaani wakati huduma za afya na usafiri zinaposimama.

Intaneti kama Silaha vs Intaneti kama Huduma

Uganda imeweka wazi kuwa kudhibiti kasi ya mawasiliano wakati wa michakato nyeti ya kitaifa, kama uchaguzi, si kunyima uhuru, bali ni hatua ya dharura ya usalama kuzuia uzushi kwani katika kilele cha taharuki, mitandao hujaa taarifa zisizothibitishwa zinazoweza kuchochea mauaji na uporaji.Aidha htua hizi huzuia matokeo yasiyo rasmi kusambaa na kuleta vurugu kabla ya mamlaka kutoa tamko la mwisho.

Mifano kutoka Kenya (Juni 2024), Senegal, na hata Bangladesh wameonesha kuwa usumbufu wa intaneti unatumika kama "breki" ya kuzuia nchi isitumbukie kwenye machafuko yasiyoweza kurekebishika.

Ni dhahiri katika hili thamani ya maisha ya binadamu haiwezi kupimwa kwa GB za intaneti. Machafuko yanapotokea akina mama wajawazito na wagonjwa wa dharura hushindwa kufika hospitalini kutokana na barabara kufungwa huku watoto wanaoshuhudia mauaji mitaani wakipata makovu ya kisaikolojia yanayozalisha kizazi chenye chuki.

Pia kunapozuka vurugu uchumi husimama kwani hakuna mwekezaji anayeweza kuamua kuleta mitaji yake kwenye nchi inayowaka moto kwa sababu tu ya "uhuru wa habari za uzushi."

Tanzania na Diplomasia ya Utulivu

Tanzania inaiambia dunia kuwa imejifunza kutokana na makosa ya wengine. Katika kuelekea Dira ya 2050, serikali haitaruhusu "uhuru wa kidijitali" utumike kuua misingi ya utu na amani iliyojengwa kwa miongo mingi.

"Hakuna mabadiliko ya kisiasa yanayostahili kulipiwa kwa uhai wa raia wasio na hatia," ni ujumbe uliosimama imara,Tanzania inasonga mbele kwa kauli moja: Internet is a tool, but Peace is a Treasure.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com