
Na Mwandishi wetu,
Wakulima wameyasema hayo leo tarehe 16 Januari 2026 mbele ya Afisa Tarafa Lisekese Emmanuel Shilatu alipo watembelea Wakulima Mashambani maeneo ya Kijiji cha Lukuledi B Kata ya Lukuledi kujionea hali ya Kilimo na kusikiliza na kutatua changamoto zao.
"Sisi Wakulima hatuna mashaka, mazao yamestawi na tunatarajia kupata mavuno mengi sana mvua zikiendelea kunyesha yatakayo pelekea kuwa na Chakula kingi na Cha akiba pia. Kwa ujumla tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia pembejeo kama vile Dawa na Mbegu zinazotupa faraja na hakikisho la Kilimo",alisema Mkulima Yonas Edwin.
Akizungumza na Wakulima mbalimbali Shilatu aliwapongeza Wakulima hao na kuwapa angalizo la kuhifadhi Chakula.
"Nimekuja kuwatembelea kama ilivyo desturi yangu, nawapongeza Wakulima wote wa Tarafa yangu kwa kazi nzuri ya kulima na jambo la kufurahisha Wakulima wengi ni Vijana mmeamua kuwekeza kwenye Kilimo, hongereni sana. Najua uhakika upo wa mavuno mazuri kwa ajili ya Chakula na biashara. Angalizo msisahau kuweka akiba ya Chakula". Alisema Shilatu.
Naye Afisa Kilimo Kata Bi. Kuruthum amebainisha bayana endapo mvua zitaendelea kunyesha Wakulima wanatarajia kupata mavuno mengi kwani hatua za awali mazao yametoa dalili njema.
Maeneo mbalimbali kumekuwa na mvua zilizonyesha na Wakulima wametumia mvua hizo kulima mazao ya muda mfupi kama vile Mahindi, Mbaazi, Alizeti, Ufuta na Karanga.


Social Plugin