Na Danson Kaijage,Chamwino
BAADHI ya wakazi wa Kata ya Buigiri na Chamwino Mkoani Dodoma wameupongeza uongozi wa halmashauri ya Chamwino kwa kuona umuhimu wa kupima maeneo yao.
Mmoja wa wamiliki wa mashamba ya chamwino Keneth Willison amesema kuwa ni furaha kubwa kwa wana Buigiri kupata mradi wq upimaji wa ardhi ili waweze kumilikishwa ardhi.
Willison amesema maeneo ya Buigiri imekuwa ikikabiliwa na changamoto kushindwa kupimiwa na kusababisha maeneo hayo kushindwa kutumika kikamilifu kwa madai kuwa maeneo hayo yalikuwa ni matumizi ya bonde kwa misingi ya Vyanzo vya maji.
"Tunaushukuru uongozi wa halmashauri ya chamwino kuona umuhimu wa kupima ardhi na kutaka kuwamilikisha wqnanchi ili waweze kutumia maeneo hayo kwa mpangilio unaokubalika jambo ambalo litawasaidia wananchi kuwa na maendeleo"ameeleza Willson.
Kwa upande wake Elizabeth Mtomo anesema kuwa kitendo cha halmashauri kuanza upimaji wa ardhi utasaidia wananchi kupata ardhi ambayo itatunika kwa mpangilio mzuri.
"Tunashukuru halmashauri kuanza zoezi la upimaji tunaamini sasa tutakuwa mpangirio mzuri na kuwa na ujenzi mzuri wa majengo huku tukiamini kuwa sasa tutakuwa wamiliki harari na wenye furaha na ardhi yetu"ameeleza Elizabeth.
Mwananchi huyo pia amewataka wanachi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upimamaji na urasimishaji ardhi kwa nia ya kumilikishwa makazi,biashara na maeneo ya taasisi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino Mkoani Dodoma Tito Mganwa amesama kuwa halmqshauri imetoa elimu kwa wamiliki wa ardhi kwa wakazi wa Chamwino na Buigiri juu ya upimaji wa ardhi inayopata kuwa hekari 1000.
Lengo la kupima ardhi ni kuhakikisha wananusuru chanzo cha maji ambacho kinaweza kuvamiwa na watu huku wakitaka kila mwenye ardhi arasimishwe eneo laki.
Tito ameeleza kuwa mpango huo wa kupima maeneo kutasaidia kuondokana na migogoro ya ardhi na kuwataka kujenga mji wa chamwino kwa mpangirio unaokubalika kisheria.
Hata hivyo ameeleza kuwa wananchi wote watakaokuwa wamepimiwa watakuwa nanuhuru wa kuripia gharama ya upimaji na atakayeshindwa kulipia ni wazi kuwa watalipwa fidia na halmashauri bila dhuruma yoyote.
Kwa upande wake Diwani wa Buigiri Keneth Yindi amewatoa hofu wakazi wa maeneo hayo kwa kusema kuwa upimaji utazingatia haki na utu.
Yindi ameeleza kuwa wananchi wote watakaopimiwa watakuwa na uhakika wa kumiliki maeneo yao na wale watakao shindwa kulipia gharama za upimaji ni wazi Halmashauri itawalipa fidi bila utata wowote.



Social Plugin