Wadau zaidi ya 100 kutoka taasisi za serikali, mamlaka za bandari na usafiri, sekta binafsi ya usafirishaji, waagizaji, wauzaji nje na wamiliki wa mizigo wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili ufanisi wa bandari pamoja na uendelevu wa uendeshaji wake kupitia ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (PPP).
Mkutano huo wa majadiliano umelenga kubaini changamoto zinazoikabili biashara na usafirishaji katika bandari za Tanzania, pamoja na kujadili suluhisho za vitendo kupitia ushirikiano wa sekta hizo mbili ili kuwezesha biashara na kuendeleza miundombinu ya bandari.
Wadau hao wameitaka Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa kupunguza gharama za usafirishaji, sambamba na kuhakikisha rasilimali za bandari zinawanufaisha wananchi na si tu wawekezaji.
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ushirikiano wa Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila, alisema sekta ya bandari na usafirishaji ni nguzo muhimu ya uchumi wa Taifa na inaweza kutoa mchango mkubwa zaidi katika ukuaji wa uchumi endapo itawekewa uwekezaji wa kutosha.













Social Plugin