Kanali mstaafu Hamis Mayamba Maiga Mkuu wa Wilaya ya Missenyi ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa akizungumza
Nahson Sigalla Mkurugenzi udhibiti uchimi TASAC akizungumza

Na Mbuke Shilagi Kagera.
Kanali mstaafu Hamis Mayamba Maiga Mkuu wa Wilaya ya Missenyi ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amewashukuru Wakala wa Meli Tanzania TASAC kwa kuandaa mkutano wa wadau wa usafiri na usafirishaji wa mizigo katika Meli mpya ya Mv. mwanza kwa njia ya Bukoba - Mwanza.
Akizungumza leo Desemba 19,2025 katika Mkutano wa wadau kwaajili ya kupokea maoni kuhusu maombi ya nauli za abiria na mizigo kwa Meli mpya ya Mv. Mwanza kwa njia ya Bukoba - Mwanza yaliyo wasilishwa na TASHICO katika ukumbi wa ELCT uliopo Manispaa ya Bukoba Kanal Maiga amesema kuwa serikali ilitoa Tsh. Bilion 40 kwa ajili ya kuboresha bandari za Bukoba na Kemondo.
Amesema kuwa meli mpya ya Mv. Mwanza imegharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 125.5 za utengenezaji ambapo itatoa fursa za shughuri za kibiashara kama samaki, mazao ya kilimo na biashara ndogo ndogo ambazo zinategemea usafiri wa majini.
Aidha Kanal Maiga mesema kuwa kupitia mkutano huo wadau watatoa mapendekezo ya nauli, ikiwa lengo nikuwa na meli inayokuwa na viwango vya nauli ambavyo ni nafuu kwa watumiaji ili kuwawezesha kuitumia lakini pia kuwezesha huduma za Meli hiyo kuwa endelevu.
Ametoa wito kwa viongozi wa kampuni ya Meli Tanzania kuangalia uwezekano na Meli hiyo kutoa huduma Nchi jirani kama vile Uganda na Kenya ambayo itaweza kuchechemua uchumi wa Kanda ya Ziwa hususani Mkoa wa Kagera.
Amesema ni matumaini yake kuwa mkutano huo utakusanya maoni tu bila kufanya maamuzi ambapo baada ya kukusanywa na kuchakatwa mdhibiti atatoa uamuzi kuhusu viwango vinavyostahili ambapo maamuzi hayo yatapita ngazi mbalimbali serikalini na umma utatangaziwa kuhusu viwango rasmi vya nauli vitakavyotozwa na TASHICO kwa abiria na mizigo inayosafirishwa na Meli mpya ya Mv. Mwanza.









Social Plugin