Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MWASSA : MAZINGIRA WEZESHI SIRI YA MAFANIKIO YA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIJANA KAGERA

Na Mbuke Shilagi Kagera. 


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa siri ya vijana wengi kufanikiwa katika mikopo ya asilimia 10 ni kutoanza kwa kutoa pesa tasirimu bali wanaanza nakuweka mazingira wezeshi.

Ameyasema hayo leo Desemba 19,2025 katika kongamano la Uwekezaji Kagera lililofanyika katika ukumbi wa KCU ulipo Manispaa ya Bukoba ambapo amesema kuwa baada ya kutoa mazingira wezeshi utekelezaji huanza kwa makundi na mikopo hutoka kisha ufatiliaji na tathimini hufuata.

Rc Mwassa ameongeza kuwa kwa vijana wa Mkoa wa Kagera waliwaombea trekta tano na Wizara ya Kilimo ambazo zipo katika halimashauri ambazo huwaandalia shamba na baada ya kuwaandalia kila kijana anapata heka moja ambalo atapanda kuweka mbolea kumwagilia na kuweka nyasi.

Ameongeza kuwa vijana hao wanapewa heka moja kila kijana mmoja ili kuwapa vijana wengi fursa ambapo amesema kwa endapo kijana atalima vizuri kiwango cha chini heka moja inazalisha shilingi milion 12. 

Amesema vijana ni asilimia 34 na ni nguvu kazi na ni theruthi moja ya nguvu kazi ya Taifa ni lazima kuhakikisha wako kazini huku akihakikisha kuwa nguvu kazi hiyo itazalisha na ataweka mazingira wezeshi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com