Na, Ruth Kyelula, Manyara RS.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe Queen Sendiga, amefanya ziara ya ukaguzi wa muradi, kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, ambapo ameanza ziara yake hiyo ya Kata kwa Kata, yenye kauli mbiu "tunavua buti ama hatuvui, tukutane site".
Ziara hiyo imefanyika Desemba 04, 2025, katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', ambapo ameambatana na Wakuu wa Taasisi zote za Umma na binafsi za Mkoa wa Manyara.
Katika ziara yake hiyo ya siku tatu, amefanya ukaguzi wa mradi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Hanang',ameweka jiwe la msingi shule ya awali na msingi Semonyan iliyopo Kata ya Mogitu, amekagua ujenzi wa mradi wa shule mpya ya Sekondari Waret.
Pia, amekabidhi nyumba kwa mwathirika wa maporomoko ya tope la Desemba 03,2023, amefanya mkutano wa hadhara Waret, amekagua madarasa mawili shule ya msingi Gisamjanga, amekagua ujenzi wa mradi wa bweni la wavulana shule ya sekondari Mwahu,na amefanya mkutano wa hadhara kijiji cha Gehandu.
Aidha RC Sendiga, katika ziara yake hiyo ya ukaguzi wa miradi na kusikiliza kero, ametoa wito kwa wananchi kupanda miti ya kivuli na miti ya matunda maeneo yote ya miradi na miradi ya ujenzi wa shule, ikamilike kwa wakati ili mwezi Januari watoto waingie shule.



Social Plugin