Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MATESO NA MADHARA YA VURUGU NI MAKUBWA, TUSIRUDIE YA OKTOBA 29- SIMBACHAWENE



Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. George Boniface Simbachawene ametoa rai kwa wananchi wa Tanzania kuipenda nchi yao na kutokubali kujirudia tena kwa matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

Mhe. Simbachawene amebainisha hayo leo Jumatatu Disemba 08, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar Es Salaam, akisema maandamano haramu ama fujo zimekuwa tabu na mateso kwa watu wengi wasiohusika wakiwemo watoto.

"Nichukue nafasi hii kuwatakia kila la kheri kwenye sikukuu hizi za mwisho wa mwaka, tukianza na kesho ambayo ni siku ya kusherehekea miaka 64 ya uhuru na ni imani yangu kwamba wananchi mmejua adha na mateso mliyoyapata na ambayo mtaendelea kwa madhara tu ya tarehe 29. Sasa tusirudie tena haya na mimi na wenzangu tunawaomba sana tuipende nchi yetu."




"Mashabiki wengi wanaosuka hii mipango na kufanya wengi wao hawapo hata hapa nchini na wale walioko hapa pengine wamechoka na hii hali lakini tunaowamba sana, tulio wengi tumeona madhara yake, madhara ni makubwa sana, mateso ni makubwa na walioathirika si tu waliojihusisha na maandamano."

Aidha Simbachawene ameeleza kuwa madhara ya vurugu hizo yamekuwa ya muda mrefu pia kiuchumi na kijamii, akitumia nafasi hiyo pia kuwatakia wananchi wa Tanzania kheri ya sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo Krismasi na Mwaka mpya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com