
Gari ya umeme
Utulivu wa Tanzania tangu uhuru mwaka 1961 umeifanya nchi kuwa kitovu cha utaalamu kikanda. Hivi karibuni, wataalamu 12 wa uvuvi kutoka Somalia wamehitimu mafunzo ya Tathmini ya Wingi wa Samaki (Fish Stock Assessment) yaliyoendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI).
Kwa Somalia kuichagua Tanzania na TAFIRI badala ya mataifa mengine, ni ishara ya imani kubwa katika utaalamu na amani yetu.
Katibu Mkuu, Agnes Meena, amesisitiza kuwa mafanikio haya ni matunda ya Serikali tulivu ambayo sasa inasafirisha maarifa kusaidia mataifa yenye mahitaji ili kuimarisha uchumi wa buluu barani Afrika.
Mazingira Tulivu Yavutia Teknolojia ya Magari ya Umeme (GAC)
Amani na mahali ilipo Tanzania (Strategic Location) vimeendelea kuwa kivutio kwa wawekezaji wakubwa. Kampuni ya magari ya GAC kutoka China imechagua kuanzia Tanzania katika kanda ya Afrika Mashariki kuingiza magari ya kisasa yanayotumia umeme na yale ya mfumo pacha (Hybrid).
Magari haya yanayoweza kusafiri kilometa 500-600 kwa chaji moja, yanatajwa kupunguza gharama za maisha kwa asilimia 300 ikilinganishwa na magari ya kawaida.
Uwepo wa bandari za Dar es Salaam na Mtwara unaiweka Tanzania kuwa kitovu cha usambazaji wa teknolojia hii kuelekea nchi jirani, jambo ambalo linafungua fursa lukuki za ajira na utaalamu kwa vijana wetu.
Wananchi wamehimizwa kutambua kuwa Tanzania ni nchi ya umma inayoongozwa kikatiba na kisheria. Tunapodai haki, ni lazima tuikumbuke amani kama chombo pekee cha mazungumzo. Vurugu na maandamano ni urithi wa maumivu, lakini amani ndiyo iliyotuletea miradi kama ya Bandari ya Karema, teknolojia ya GAC, na heshima ya kutoa mafunzo kwa nchi kama Somalia.
"Sisi kama Watanzania hatuko tayari kuona nchi yetu inayumbishwa na wachache wasioitakia mema. Kama huna uchungu na Taifa hili, usivuruge amani inayotuletea wawekezaji na kutuongezea heshima kimataifa."
Afya ya Akili na Ustawi wa Jamii
Katika kuelekea maendeleo haya, jamii imekumbushwa pia umuhimu wa utulivu wa kisaikolojia. Maendeleo ya nchi yanahitaji watu wenye akili timamu, wasio na msongo wa mawazo wala hofu. Huduma za Saikolojia Tiba sasa zinapatikana kwa gharama nafuu ili kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na utulivu wa ndani utakaomwezesha kushiriki katika ujenzi wa Taifa na kutumia fursa za ajira zinazojitokeza kupitia uwekezaji wa GAC na sekta ya uvuvi.
Tanzania inaposonga mbele kwa kasi chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Amani yetu ndio mtaji wetu mkuu. Tusiichezee, bali tuitumie kama chachu ya kufikia Dira ya 2050 na kuimarisha nafasi yetu kama kiongozi wa maendeleo na amani katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Social Plugin