Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMANI NA UTULIVU VYATAWALA SIKUKUU YA KRIMASI DAR ES SALAAM



Maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wameendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali Jijini hapa kwaajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, iliyo maarufu zaidi kwa waumini wa dini ya Kiikristo kote ulimwenguni ikiwa leo ni siku ya pili maarufu kama Boxing day, siku maalum kwaajili ya kupeana zawadi za Krismasi.

Suala la amani, utulivu na usalama limeshuhudiwa pia katika maeneo yenye misururu ya watu ikiwemo kwenye Fukwe za Coco (Coco Beach), Wilayani Kinondoni pamoja na eneo maarufu la Mlimani city.

Katika fukwe hizo, Polisi wameonekana wakfanya doria za mguu, farasi pamoja na magari ili kuhakikisha kila mmoja anasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu, wananchi wakiipongeza serikali na polisi kwa kuhakikisha amani inaendelea kuwepo.

Kwa nyakati tofauti mara baada ya kushindwa kwa upangaji, uratibu na ufanyikaji wa maandamano yaliyokuwa haramu hapo Disemba 09, 2025, baadhi ya wanaharakati walikuwa wakihamasisha maandamano hayo kufanyika katika sikukuu hii, kabla ya kupingwa na kukataliwa kwake kulikofanywa na Watanzania wenye kutambua na kuhamasisha zaidi umuhimu wa amani na utulivu kwa mustakabali wa maendeleo na ustawi wa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com