Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAGERA YANG'ARA MAONESHO YA TAMADUNI MBALIMBALI KILELE IJUKA OMUKA


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa (kulia) akiwa na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. George Simbachawene (aliyevaa miwani) na viongozi wengine wakila chakula cha asili

Na Mbuke Shilagi Kagera. 

Kilele cha Tamasha la Ijuka Omuka msimu wa tatu 2025 lenye kauli mbiu ya wekeza Kagera irudishe katika ubora wake kimehitimishwa kwa maonesho mbalimbali ya tamaduni.

Kilele cha Tamasha hilo kimefanyika leo Desemba 21,2025 katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba ambalo limejumuisha vyakula vya asili,ngoma za asili,mila na desturi za makabila yanayopatikana Mkoa wa kagera,utamaduni wa buhaya na historia ya kuanguka na kuinuka kwa ngome ya Buhaya.


Aidha viongozi mbalimbali wameshiriki Tamasha hilo ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri  wa Mambo ya Ndani George Simbachawene,Naibu Mkurugenzi kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Julieth Kabyemela,Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Hajjat Fatma Mwassa, Viongizi wa Serikali,Viongozi wa Dini,Viongozi wa kisiasa Mkoa,Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa pamoja na Taasisi za Umma na binafsi. 













Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com