Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU AWASILISHA UJUMBE WA RAIS SAMIA MAADHIMISHO YA MIAKA 64 YA UHURU


Waziri Mkuu, Mh. Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuelekea maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania yanayofanyika Desemba 9, 2025.

Akizungumza leo Desemba 8, 2025, Dkt. Nchemba amesema Rais Samia anawatakia Watanzania wote sikukuu njema ya Uhuru, akisisitiza umuhimu wa kuienzi kwa kufanya shughuli za amani, utulivu na mshikamano.

Amesema, “Ndugu wananchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawatakia Watanzania wote sikukuu ya Uhuru wa Tanzania inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Desemba.”

Aidha, Serikali imewataka wananchi wote ambao hawatakuwa na dharura au ulazima wa kuwapo kazini, kutumia siku hiyo kupumzika na kuadhimisha sherehe hizo wakiwa majumbani, isipokuwa wale watakaolazimika kuwepo kwenye vituo vyao kwa mujibu wa majukumu yao ya kila siku.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com