
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameweka jiwe la msingi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kampasi ya Kagera kilichopo katika vijiji vya Kangabusharo na Itahwa Kata ya Karabagaine Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambapo ameawagiza wanao husika na mradi huo hususani wahandisi,washauri wa ujenzi,wakandarasi na wasimamizi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Akizungumza leo Desemba 15,2025 katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi iliyofanyika katika chuo kikuu cha Dar es salaam kampasi ya Kagera Balozi Dkt. Nchimbi ameiagiza Wizara ya elimu kwa kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha taratibu na mahitaji mengine muhimu ikiwemo ithibati,vifaa,rasilimali watu na mipango ya matumizi imeandaliwa mapema ili kuwezesha shughuli za kampasi mpya kuanza pasipo na vikwazo.
Naye Mkuu wa chuo na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameomba kuongezewa ardhi kwa mahitaji ya chuo ya sasa na miaka ijayo ambapo amesema siku za mbeleni kampasi hiyo itakuwa chuo kikuu katika Mkoa wa Kagera huku akiomba serikali kuendelea kuzungumza na Ba
Benki ya Dunia ili kupata fedha kwa awamu ya pili, pia serikali kusaidia kujenga mabweni ya vijana wa kiume pamoja na kamuomba Makamu wa Rais kujenga barabara ya rami inayotoka barabara kuu mpaka chuoni hapo.
Balozi Dkt. Nchimbi amesema suala la bweni la vijana wa kiume kwa wanachuo amelichukua kwa uzito huku akisema kuwa Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anakifatilia chuo hicho kwa ukaribu sana na kuahidi kufikisha maombi yote kwake.
Aidha upande wa kuongezewa ardhi ya chuo amemwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa kulifanyia kazi kama alivyofanya kwa weledi mkubwa awamu ya kwanza.
Mh. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameambatana na Mkuu wa chuo na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Adolf Mkenda {mb} pamoja na viongozi mbalimbali wa Siasa na Serikali wa na wakuu wa idara wa Wilaya na Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama.








Social Plugin