Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo daktari Juma Zuberi Homera akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza jimboni humo
Na Regina Ndumbaro-Namtumbo Ruvuma
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Dkt. Juma Zuberi Homera ameendelea kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo jimboni humo baada ya kuleta mpango mkubwa wa kuanzisha kilimo cha kakao na kufufua upya kilimo cha tumbaku katika vijiji vya Msisima, Magazini na Sasawala.
Homera amesema kuwa kilimo cha kakao ni cha thamani kubwa kwani kilo moja ya zao hilo huuzwa kwa shilingi 15,000, huku miche elfu arobaini ikinunuliwa kutoka mkoani Mbeya kwa ajili ya wakulima wa Namtumbo.
Aidha, Dkt. Homera amesema kuwa vitalu vya miche ya tumbaku tayari vimetengwa na vimeanza kupandwa,
huku akiongeza kuwa tani 3000 za mbegu za ufuta zipo tayari hivyo wananchi ni maamuzi yenu kuchagua mnataka kulima zao lipi kati ya ufuta , mbaazi au mahindi huku akiwaahidi kundi la vijana kuwalipia hekari tano wazee na akina mama
Homera amesema pia nilichokipata lazima tugawane na nyinyi wananchi na ndio maana nikaona nikimbie mara moja nyumbani kuongea na nyinyi ili kuhakikisha yale yaliyoahidiwa yaanze kufanyiwa kazi
Amesisitiza kuwa ataendelea kusimamia kwa karibu masoko ya mazao hayo ili kuhakikisha wakulima wanapata malipo yao kwa wakati na kunufaika na jitihada zao.
Amezitaka kata 21 na matawi 132 jimboni humo kuchangamkia fursa hiyo akisema kuwa "kilimo ni uti wa mgongo" na kuhamasisha wananchi kujikita shambani badala ya kushawishika na uzushi wa mitandaoni unaohusu maandamano.
Katika kuimarisha miundombinu, Waziri Homera amesema ukarabati wa daraja la Namali unaendelea vizuri baada ya daraja hilo kuwa na changamoto kubwa wakati wa misimu ya mvua.
Ameeleza kuwa ukarabati huo ni miongoni mwa jitihada za serikali kuboresha upatikanaji wa huduma na kurahisisha usafiri kwa wananchi.
Dkt. Homera ametoa wito kwa viongozi, madiwani, wajumbe na wananchi kushirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleo na mabadiliko makubwa ndani ya Jimbo la Namtumbo.
Amesema kuwa ushirikiano huo ni msingi muhimu katika mafanikio ya miradi ya kilimo na miundombinu inayotekelezwa kwa maslahi ya wananchi wote.

Social Plugin