Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI 18 KISHAPU WAKABIDHIWA HATI MILIKI BAADA YA KUPISHA MRADI WA UMEME JUA NGUNGA

Na Sumai Salum – Kishapu

Jumla ya wananchi 18 waliopisha mradi mkubwa wa maendeleo wa Umeme Jua (Solar Power Project) eneo la Ngunga, Kata ya Talaga, Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamekabidhiwa hati miliki za ardhi kama sehemu ya fidia na utaratibu wa kuwawezesha kumiliki maeneo yao kisheria.

Akikabidhi hati hizo Novemba 27, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter N. Masindi, amesema umiliki wa hati ni jambo muhimu kwa kila mwananchi, siyo tu kwa waliolipwa fidia, kwani hati huongeza thamani ya ardhi na kuleta uhakika wa usalama wa mali.

“Ukiwa na hati, eneo lako linaongezeka thamani. Hakikisheni mnatunza nyaraka hizi vizuri, kwani ni muhimu kwenu na kwa vizazi vyenu vijavyo,” amesema Mhe. Masindi.

Aidha, amewapongeza wananchi hao kwa kukubali maendeleo kwa kuachia maeneo yao kupisha mradi huo mkubwa, huku akiwashauri kutumia fursa iliyotokana na uwekezaji huo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo nyumba za kupangisha na huduma za malazi kutokana na ongezeko la watu katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Shinyanga, Bw. Leo Komba, amesema fidia ya mradi huo imekuwa ya mfano kwa kuwa kila mwananchi alipewa uhuru wa kuchagua eneo analotaka kuhamia, kisha kununuliwa na kukabidhiwa hati miliki.

“Mradi huu una jumla ya ekari 1,200 na wananchi waliopisha ni 98. Wengi waliamua kuhamia nje ya Kijiji cha Ngunga, na wote tumewatafutia maeneo kulingana na matakwa yao kisha watapatiwa hati miliki za maeneo hayo,” amesema Komba.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Karaba Mpange amepongeza juhudi za serikali kwa kuwathamini kwani jambo Hilo limekuwa chachu kwao kutokana na kutokuwa na hatimilki ya maeneo Yao na bado serikali ilipoomba kuanzisha mradi ikawatafutia maeneo mengine na kuwapa uhalali wa kisheria.

"Kiukweli kuwa na hati kwetu ilikuwa ni ndoto ya alinacha, hatukuwa na haya maono kabisa na hata sasa tunazaidi ya miaka 50 ya umri, tunaishukuru sana serikali hii ya awamu ya sita kwa kutufanya tujisikie wa thamani katika Taifa letu kwa kutupa fidia hii mapema huku ikizingatia kanuni na sheria za ulipwaji fidia wa kitafa na kimataifa" ameongeza Mpange

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya mapema wiki hii amefanya vikao na viongozi wa makundi mbalimbali ya wananchi kujadili maandalizi ya msimu wa uzalishaji (kilimo) na masuala ya amani. Alihutubia viongozi wa dini, watendaji wa vijiji, kata na vitongoji, viongozi wa bodaboda, wazee maarufu na wazee wa kimila kutoka tarafa za Mondo, Negezi na Kishapu.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Peter N. Masindi akizungumza kwenye zoezi la ugawaji hati miliki kwa wananchi waliopisha mradi wa umeme jua kijiji cha Ngunga wilayani humo Novemba 27,2025
Kamishina wa ardhi Mkoani Shinyanga Leo Komba akizungumza kwenye ugawaji hati miliki kwa wananchi waliopisha mradi wa umeme jua kijiji cha Ngunga wilayani humo Novemba 27,2025

Afisa tarafa ya Negezi Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Tano Malele

Kaimu afisa ardhi Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Grace Pius akizungumza

Kaimu Mtendaji Kata ya Talaga Mussa Emmanuel akizungumza

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mussa Masesa akizungumza

Mwakilishi wa wananchi Karaba Mpange akishukuru
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Peter Masindi akimkabidhi hatimiliki ya ardhi Dotto Paul Mganga

Mkuu wa Wilaya ya kishapu Mhe.Peter Masindi akimkabidhi hatimiliki ya ardhi Sunga Mpendazoe 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Peter Masindi akimkabidhi hatimiliki ya ardhi Mahola Mpange Shimba 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Peter Masindi akimkabidhi hatimiliki ya ardhi Peter Timotheo Mwandu 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Peter Masindi akimkabidhi hatimiliki ya ardhi Masunga Mwandu Cheyo 

































Picha za ziara ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Masindi Tarafa ya Kishapu, Negezi na Mondo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Peter N. Masindi akizungumza kwenye ziara yake
Katibu Tawala Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohammed
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson












Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com