Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WALIOHARIBIWA BIASHARA ZAO WAMERUDISHWA NYUMA KIUCHUMI




Na Mwandishi wetu,DAR

Baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam wameeleza masikitiko yao kufuatia vitendo vya uvunjwaji wa biashara na uharibifu wa miundombinu ya Serikali vilivyotokea kuanzia siku ya kupiga kura.

Wamesema vitendo hivyo ni vya kihalifu na vimefanywa na watu wachache wenye nia ovu, huku wakibainisha kuwa athari zake zimekuwa kubwa kwa wajasiriamali wadogo ambao sasa wamerudi nyuma kiuchumi baada ya kupoteza mitaji na mali zao.

Aidha, wananchi wameitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika ili kulinda amani na kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelea kwa utulivu katika jiji hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com