Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUENDELEZA KILIMO IKOLOJIA NCHINI


Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Kilimo,Stephen Nindi akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa mbegu za asili na matumizi yake kutoka mkulima Mary Mbaga anayezalisha mbegu hizo wilaya ya Same Kilimoanjaro,katika maadhimisho ya miaka 30 ya Pelum Tanzania.
Mratibu wa Shirika la Participatory Ecological Land Use Management Tanzania ,Donath Senzia akiongea na wadau mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya miaka 30 ya  Pelum Tanzania.

***
SERIKALI  kupitia Wizara ya Kilimo inaweka mikakati ya kuendeleza Kilimo Ikolojia kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa kilimo  likiwemo Shirika la Participatory Ecological Land Use Management (PELUM),Tanzania ili kufanya kilimo  chenye kuleta tija  kwa wakulima na kuinua uchumi wa Taifa.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Stephen Nindi alisema hayo wakati akifungua maadhimisho ya miaka 30 ya Pelum Tanzania,ambapo alieleza kuwa, mchango wa taasisi zisizo za kiserikali unatambulika na serikali.

 "Natambua Pelum katika kipindi cha miaka 30 iliyopita imepata mafanikio makubwa na kati ya hao ni kushiriki wenu wa kikamilifu katika uandaaji wa sera mbalimbali , sheria , mipango na mikakati katika sekta ya kilimo na ardhi maeneo ya vijijini", alisema  Dk. Nindi.

Dk Ndindi pia alisema Wizara itaendelea kushirikiana na Pelum Tanzania na wadau wengine wa mbegu za asili katika kuandaa usajili wa mbegu za asili za wakulima ambapo hadi sasa kuna mbegu 13 zimesajiliwa  na hivyo kutambulika kisheria.

Naibu Katibu Mkuu  alibainisha kuwa , Wizara pia itajenga Benki ya vinasaba vya mbegu kwa kushirikiana na wadu wa kilimo ikilojia katika kuhifadhi , kuendeleza bauonuai za mbegu za asili 

Dk. Nindi alisema hatua hiyo ya kushirikiana na wadau wa kilimo ikolojia,itaendelea kusimamia na kuhamasisha kilimo hicho ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo alisema kuwa jitihada hizo zitasaidia kuongeza uzalishaji na tija katika mazao na kuwezesha kuimarisha usalama wa chakula nchini na pia kuimarisha kipato cha wakulima.

Mratibu wa Pelum Tanzania,Donath Senzia alisema katika kipindi cha miaka 30 wamefanikiwa kujenga osifi kwa thamani ya shilingi bilioni 1.4,hivyo kuondokana na changamto ya kodi,na kuweka mazingira salama ya watumishi kufanya kazi.

Alisema Pelum Tanzania imeshiriki kikamilifu katika uandaaji wa sera, sheria na mikakati mbalimbali ya kilimo na ardhi ikijumuisha sera ya taifa ya kilimo, sera ya ardhi, sheria ya ardhi, kanuni na miongozo za kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji, mpango mkakati wa kilimo ikolojia hai, sheria ya mbegu, muongozo wa uzalishaji wa mbegu za wakulima.

Mkulima kutoka mkoa wa Kilimanjaro,Mary Mbaga alisema  matumizi ya mbegu za asili yamemsadia kuinua kipato chake,kusomesha watoto na kuendeleza familia yake kwa kufanya kilimo kwa kutumia mbegu za asili.
Mary alisema  kilimo cha kutumia mbegu za asili wingi wa mazao unaongezeka na kufanya mkulima kuuza na kupata kipato,kwani mbegu za asili bado zina ubora mkubwa na zinatunza ardhi katika kurutubisha rutuba iliyopo kwa kipindi cha muda mrefu kuliko zisizo za asili.
 
“Matumizi ya mbegu za asili na kilimo ikolojia vina nafasi kubwa katika jamii,humsaidia mkulima kuweza kukidhi mahitaji kwa kuuza mazao,tunaozalisha na kutumia mbegu za asili hatukosi chakula nyumbani katika misimu yote”,alisema Mary.
 
Hivyo aliiomba Serikali  kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo kuwekeza katika  kuzitangaza mbegu za asili,kutambua wazalishaji wa mbegu za asili ambao wengi wao wanaishi maeneo ya vijijini na mchango wao ni mkubwa katika sekta ya uzalishaji chakula ndani ya nchi na nje ya nchi.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com