

Shule ya Msingi Samuu Primary School iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imefanya vizuri kwa kiwango cha juu katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba (PSLE) mwaka 2025, baada ya wanafunzi wake kufaulu kwa asilimia 100 na shule hiyo kupata Daraja A (Bora).
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), jumla ya wanafunzi 63 walifanya mtihani huo na wote wamefaulu kwa mafanikio makubwa, huku shule ikipata wastani wa alama 272.3968.
Kati ya wanafunzi hao, wasichana 28 na wavulana 35 walishiriki mtihani, ambapo wanafunzi 59 wamepata daraja A, na wanafunzi 4 wakipata daraja B. Hakuna mwanafunzi aliyepata daraja C, D au E – ishara kwamba shule hiyo imejipambanua kuwa miongoni mwa shule bora zaidi katika Mkoa wa Shinyanga na hata kitaifa.
Mafanikio hayo yanatajwa kuwa matokeo ya juhudi kubwa za walimu, ushirikiano mzuri wa wazazi pamoja na nidhamu na bidii ya wanafunzi, chini ya uongozi makini wa walimu wakuu wa shule hiyo.
Wazazi na wananchi wameipongeza shule hiyo kwa kuendelea kuwa kielelezo cha ubora wa elimu, huku wakihamasisha shule nyingine kuiga mfano wake wa mafanikio.
Social Plugin