Mgombea
Udiwani Kata ya Maganzo Hamza Tandiko amewaomba wananchi kwenda kupiga kura
Oktoba 29 ili watimize haki yao ya msingi ya kikatiba na kuwapuuza watu
wanaosema hawapigi kura kwani hao hawajui haki yao wanatakiwa kuelimishwa .
Akizungumza
na wakazi wa Kijiji cha Masagala Kata ya Maganzo,mgombea Udiwani amesema nchi
inaamani kwani Jeshi liko imara kulinda nchi na hakuna vurugu na kuwaomba
kwenda kupiga kura siku ikifika wachague viongozi wanaotokana na chama cha
Mapinduzi ili waendeleze maendeleo.
Ametumia
mkutano huo kutoa elimu namna ya kupiga kura kuanzia Rais,wabunge na
madiwani huku akiwaomba kuhakikisha wanaweka tiki ya ndiyo nafasi ya udiwani
ili waweze kumchagua kuwa diwani wao kwa
kumpa kura nyingi za ndiyo kwa kuwa hana mpinzani isipokuwa atapigiwa kura ya
ndiyo nay a hapana.
Katibu
Mwenezi wa CCM Kata ya Maganzo Juma Rajabu amesema vurugu huwa zinachanzo chake
na kuwaomba wananchi wa Kata hiyo wasikubali kutumika na kuwa chanzo cha
uvunjifu wa amani kwa kuvunja sheria .
Amewaomba
kupuuza uzushi unaotolewa kwenye mitandao ya kijamii ambao umekuwa ukisababisha
hofu na kueleza kuwa kuna amani ya kutosha siku ya uchaguzi watapiga kura kwa
amani na kurudi nyumbani kwa amani .
Amewaomba
wazee kukaa na vijana wao kuwaonya wasijaribu kujihusisha na vurugu zozote zile
ambazo zinaweza kuachilia uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na kuepuka
kujihusisha na maandamano yasiyo ya msingi.






Social Plugin