Na Michael Abel, SHINYANGA
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, kwa kushirikiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, wametoa elimu kuhusu usalama barabarani, mbinu za uokoaji, na namna ya kukabiliana na majanga ya moto kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kolandoto, Manispaa ya Shinyanga.
Elimu hiyo imetolewa leo, Oktoba 16, 2025, katika viwanja vya shule hiyo, ikiwa ni sehemu ya kampeni endelevu ya kuwajengea uelewa vijana kuhusu masuala ya usalama na tahadhari wanazopaswa kuchukua wanapokabiliwa na majanga mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo, Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Shinyanga, Hellen Kiseru, ameeleza njia nne za kukabiliana na moto, ikiwemo kutumia vifaa maalumu vya kuzimia moto, kuzima kwa kutumia kidole endapo moto umetokana na gesi, kutumia kizimamoto (fire extinguisher) na kapeti maalum ya kuzimia moto.
Amesisitiza kuwa moto hauzimwi kwa maji bali kwa vifaa sahihi na umakini mkubwa, huku akiwataka wanafunzi kuwashauri wazazi na walezi wao kununua vifaa vya dharura kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya moto majumbani.
Kwa upande wake, Sajenti Nassor Mkongoe kutoka Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, amewafundisha wanafunzi kuhusu alama za barabarani, namna sahihi ya kuvuka barabara, na umuhimu wa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.
Naye Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Seif Nassor (RSA), amewataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri wa usalama barabarani kwa kutoa elimu waliyoipata kwa wenzao na jamii kwa ujumla, akisisitiza kuwa kufuata sheria za usalama barabarani ni hatua muhimu ya kulinda maisha na kuepuka ulemavu wa kudumu.
Katibu wa Mabalozi wa usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Chibura Makorongo akitoa elimu shule ya Sekondari Kolandoto.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Shinyanga, Hellen Kiseru akitoa elimu Shule ya Sekondari Kolandoto.
Fire Constable Erick Constantine kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Shinyanga, akitoa elimu.
Baadhi ya wanafunzi waliopatiwa elimu Shule ya Sekondari Kolandoto.
Katibu wa Mabalozi wa usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Chibura Makorongo akikabishi zawadi kutoka Jambo Food Products kwa mwanafunzi aliyeshinda zoezi la kuzima moto mara baada ya kupatiwa elimu.
Elimu ya uzimaji wa moto ikiendelea.
Elimu ya uzimaji wa moto ikiendelea.

Elimu ya uzimaji wa moto ikiendelea.
Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Seif Nassor (RSA), akizungumza wakati wa utoaji elimu kwenye shule hiyo.
Sajenti Nassor Mkongoe kutoka Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kolandoto.
Picha ya Pamoja.




















Social Plugin