Na Sifa Lubasi
WASICHANA 600 katika shule tatu za sekondari wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamepewa taulo za kike paketi 9500 .
Taulo hizo zimetolewa kwa ufadhili wa Benki ya Diamond Trust Bank ((DTB).
Wasichana wanufaika ni kutoka shule za srkondari za Chunyu, Mazae na Ving’hawe.
Mjumbe wa Bodi ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Action Girls Foundation (AGF), Dk Hawa Mkwela alisema kuwa taulo hizo zilikabidhiwa katika kueleke Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani katika shule hizo, ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 11 mwaka huu.
Akuzungumza wakati wa ugawaji wa taulo hizo kwenye shule ya sekondari ya Chunyu alisema kuwa hayo jana wakati wa ugawaji wa taulo za kike kwenye shule ya Sekondari ya Chunyu aliwataka wanafunzi hao kutumia taulo hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakitumia taulo hizo vibaya kwa kuzimwagia pombe na kuzivaa ili walewe
"Suala la matumizi ya taulo za kike vibaya Kwa kuziwekea pombe Kali na kulewa,lilibainika katika semina iliyoandaliwa na wizara ya afya ikiwahusisha wahadhiri na wakufunzi wa vyuo vikuu na kati wakati wakijadili changamoto za vijana zilizopo vyuoni zinazotokana na matumizi mabaya ya p2, vitendo kama gangsex na ulevi ," alisema.
Alisema kuwa kabla ya mpango wa kugawa taulo za kike kulikuwa na changamoto kubwa hasa za kiafya kwani maeneo mengi hasa vijijini yamekuwa na upungufu wa maji na kupelekea watoto kupata athari mbalimbali ikiwemo fangasi.
"Zamani wazee wetu walikuwa wakitumia vitambaa ambapo baadae hufuliwa vizuri na kuanikwa juani walikuwa hawapazi athari," alisema
Pia alisema kuwa awali taulo kama hizo za kufuliwa ziikuwa zikigawiwa shuleni lakini changamoto kubwa ilikuwa upatikanaji maji hasa maeneo ya vijijini na hivyo kupelekea kuwa na athari kwa watumiaji.
Alisema kuwa AGF wamekuwa na klabu za wanafunzi katika shule za sekondari wilaya ya Mpwapwa ambapo wanafunzi wanekuwa wakielimishwa juu ya hedhi salama.
Kaimu Mkurugenzi wa AGF, Wakili Fatuma Mnzava alisema kuwa dozen moja ya taulo za kike inatosha kwa msichana kujisitiri kwa miezi sita.
Alisema kuwa taulo hizo zitatosha kuwasitiri wasichana 600 kwa miezi sita,
"Wengine wanaogopa kumwambia baba ninaomba hela ya Pedi,tunatamani jambo hili liwe endelevu ili kusaidia wasichana wengi hasa wa vijijini," alisema.
Mwakilishi kutoka Benki ya DTB Lilian Kawa alisema kuwa wamekuwa wakitambua nafasi ya mtoto wa kike katika jamii.
"Kwa kutambua mchango wa watoto wa kike katika jamii tulishirikiana na AGF kuleta taulo za kike,aliongeza msome zaidi msikate tamaa ili mfikie ndoto zenu," alisema.


Social Plugin