Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHATANDA AINADI ILANI YA CCM TANGANYIKA AKIELEZA MAKUBWA YALIOTEKELEZWA NA DKT. SAMIA




Na Mwandishi wetu, Katavi

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 10 Oktoba 2025, akiwa katika Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi, kwenye Mkutano wa Kampeni, ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku akieleza mafanikio makubwa yaliyofanyika Chini ya uongozi madhubuti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine Chatanda kupitia Mkutano huo wa Kampeni, alimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanganyika, Moshi Selemani Kakoso, pamoja na Madiwani wa Kata kwa tiketi ya CCM, kupitia Jimbo hilo.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi akiwa katika Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi, ametoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya Ndiyo, licha ya uwepo kwa wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa.











Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com