
Mwakilishi kutoka Shirika la YAWE Peter Nampala akizungumza kwenye mafunzo kwa wafanyabiashara Kata ya Masekelo kupitia mradi wa kijana wajibika ijue kodi yako lipa na shiriki inayosimamiwa na shirika la YAWE

Baadhi ya wafanyabiashara wa Kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kuzitambua kodi wanazotakiwa kulipia pamoja na kueleza changamoto zinazowakabili ili zifanyiwe kazi.
****
Shirika lisilo la kiserikali la Youth and Women Emancipation (YAWE) limewajengea uwezo wafanyabiashara wa Kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga ili waweze kuelewa aina ya kodi ambazo huwa wanalipa pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili na kuweza kupatiwa ufumbuzi.
Hayo yameelezwa na mwakilishi kutoka Shirika la YAWE Peter Nampala wakati wakitoa mafunzo kwa wafanyabisha hao kupitia mradi wa kijana wajibika ijue kodi yako lipa na shiriki inayosimamiwa na shirika la YAWE.
Amesema elimu iliyotolewa itawajenga wafanyabiashara na kuwawezesha kupata uelewa wa mambo ambayo yalikuwa ni kikwazo kwenye biashara zao,hatua ambayo itawainuwa kiuchumi na kuweza kulipa kodi zao kwa wakati.


Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga kupitia dawati maalumu la uwezeshaji biashara Mkoji Wanjala akizungumza na wafanyabiashara Kata ya Masekelo.
“Leo tumekutana na wafanyabiashara wa Kata ya Masekelo ambao wamepatiwa elimu juu ya kodi ya majengo,biashara na namna ambavyo ushuru wa huduma unatakiwa kulipwa mambo ambayo wengi yalikuwa yanawasumbua lakini baada ya elimu wamepata uelewa”amesema Nampela
Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga kupitia dawati maalumu la uwezeshaji biashara Mkoji Wanjala amesema bado kuna tatizo la uelewa wa kodi wanazotakiwa kulipia ikiwemo leseni ya biashara.
Amesema uwepo wa dawati hilo litasaidia kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya kodi mbalimbali ili kuwajengea uelewa zaidi ikiwa ni pamoja na kuzifanyia kazi changamoto zilizopo ili kuweka mazingira mazuri kwa wate.


Afisa biashara Manispaa ya Shinyanga Victor Kajuna akitoa elimu ya masuala ya kodi kwa wafanyabiashara wa Kata ya Masekelo

Mafunzo yanaendelea













Social Plugin