Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhandisi James Jumbe mapema leo Oktoba 29, 2025 amejitokeza kushiriki zoezi la uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais.
Zoezi hilo amelifanya katika kituo cha kupigia kura Miti Mirefu kilichopo kata ya kambarage manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza mara baada ya kutimiza haki ya kikatiba kwa kupiga kura, Mhandisi Jumbe amesema zoezi hilo limekwenda vizuri, kwa amani na utulivu huku akiipongeza tume huru ya taifa ya uchaguzi kwa kuratibu zoezi hilo kikamilifu.
Aidha Mhandisi Jumbe ameongeza kuwa ni wajibu wa kila mtu mwenye vigezo vya kupiga kura kushiriki zoezi hilo kwani ni wajibu wa kila mtu kumchagua kiongozi atakayemuongoza kwa kipindi cha miaka 5.








Social Plugin