
Tukio hilo linatajwa kuwa miongoni mwa matamasha makubwa zaidi ya Muaythai barani Afrika, likihusisha mapambano ya hadhi ya juu yatakayojumuisha majina makubwa ya mchezo huo kutoka Sudan Kusini na Tanzania.
PAMBANO KUU (Main Event)
Nyota wa Sudan Kusini, James Majok Gau, atapanda ulingoni kupambana na bingwa wa Tanzania, Emmanuel Shija Kajala, pambano linalotarajiwa kuwa la kasi, nguvu na msisimko wa kipekee huku mshindi akinyakua mkanda wa heshima wa WBC Africa Muaythai Championship Belt.
PAMBANO LA PILI KUBWA (Co-Main Event)
Bingwa wa dunia wa Muaythai kutoka Sudan Kusini, Sky, anatarajiwa kurejea nyumbani kwa kishindo baada ya ushindi wake mkubwa nchini Thailand Novemba 2024, ambapo alimshangaza dunia kwa kumshinda bingwa maarufu wa Uholanzi. Sky atapambana na Mtanzania Musa Said Munisi, katika pambano linalotabiriwa kuacha historia kubwa kwa mashabiki wa Juba.
MAPAMBANO YA UTANGULIZI (Undercard)
Vijana chipukizi wa Sudan Kusini nao wataonesha makali yao akiwemo Simon Sudan, Abednego “Boyka” Wize J, Eddy, Rambo, John, Johnson, Classic, Irene, Thai Leng, Musa Luwate na wengineo.
VIPENGELE VYA USIKU HUO
-
Mapambano ya hadhi ya kimataifa ya Muaythai.
-
Fahari ya bara la Afrika ikijumuisha wanamichezo wakubwa.
-
Burudani, muziki na tamaduni za Sudan Kusini kuonesha mshikamano wa kitaifa.
Kwa mujibu wa waandaaji, tukio hili litakuwa zaidi ya pambano la kawaida; litakuwa ni historia inayoandikwa kwa michezo ya mapigano barani Afrika.
📍 Ukumbi: Nyakuron Cultural Centre – Juba, Sudan Kusini
📅 Tarehe: Jumamosi, Septemba 27, 2025
⚡ Kauli mbiu: WBC Africa Muaythai Championship Belt – Power. Pride. Glory. ⚡
Social Plugin