Mratibu wa Masuala ya Michezo wa kampuni ya Jambo, Crispine Kakwaya akizungumza na waandishi wa habari - Picha na Marco Maduhu
Mratibu wa Masuala ya Michezo wa kampuni ya Jambo, Crispine Kakwaya akizungumza na waandishi wa habari
Mratibu wa Masuala ya Michezo wa kampuni ya Jambo, Crispine Kakwaya akizungumza na waandishi wa habari
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Kampuni ya Jambo Group imetishia kuacha kuifadhili Timu ya Stand United iwapo haitapata ushirikiano kutoka kwa wadau wengine wa michezo mkoani Shinyanga.
Mratibu wa Masuala ya Michezo wa kampuni ya Jambo, Crispine Kakwaya, amesema leo Jumatano Septemba 10, 2025, kuwa Stand United siyo timu ya Jambo Group bali ni timu ya Wanashinyanga wote, hivyo kila mdau anapaswa kushirikiana kuiunga mkono.
“Stand United siyo timu ya Jambo, ni timu ya Wanashinyanga wote. Gharama za kuendesha timu ni kubwa, nguvu ya mtu mmoja haitoshi. Ndiyo maana tunahitaji mshikamano kutoka kwa wafanyabiashara, makampuni na migodi iliyopo Shinyanga,” amesema Kakwaya.
Amesema msimu uliopita Jambo Group ilijitahidi kuiendesha timu hiyo, lakini changamoto kubwa imekuwa kukosekana kwa ushirikiano wa pamoja, jambo linaloweza kudhoofisha ndoto ya timu hiyo kupanda Ligi Kuu.
“Kama wadau wataendelea kukaa kimya na kutochangia chochote, basi na sisi Jambo Group tutakaa pembeni. Timu hii si mali ya kampuni yetu, ni mali ya jamii nzima ya Shinyanga,” amesisitiza.
Kwa upande wao, baadhi ya mashabiki wa Stand United wameiomba Serikali iingilie kati kusaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri kwenye Ligi ya Championship na hatimaye kurejea Ligi Kuu, jambo ambalo litachochea maendeleo ya michezo na uchumi wa Mkoa wa Shinyanga.



Social Plugin