
*
Leo Septemba 18,2025 Mgombea ubunge Jimbo la solwa Ndugu Ahmed Ally Salum ameendelea na Ziara ya Kampeni Jimboni kwa kutembelea Kata ya Salawe na Solwa.
Ndugu Ahmed ameambatana na Katibu wa Vijana Mkoa wa Shinyanga Ndugu Salama Mhapi, Viongozi wa Chama wilaya shinyanga vijijini pamoja na Wateule wa Wagombea Udiwani na Viti Maalum.
Ndugu Ahmed ameahidi kutatua Changamoto za afya, Maji, Barabara, Umeme na Elimu kwa baadhi ya Vijiji ndani ya Jimbo la Solwa.
Pia ameomba kura kwa Wananchi waweze kumchagua kwa kishindo kikubwa Mgombea Urais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuharakisha Maendeleo kwa Wananchi.
Aidha Madiwani na Viongozi wamewaombea kura Wagombea wote kuanzia ngazi ya Diwani,Mbunge na Rais na kuwasisitiza Wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya Oktoba 29,2025 ili kwenda kupiga kura.
Wananchi wamekubaliana na Sera za Wagombea na kuwaahidi siku ikifika wataenda kutiki kwa *DKT Samia, Mbunge Ahmed na Madiwani.
Mwisho
KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE
#ChaguaCCM
#ChaguaSamia
#ChaguaAhmed
#Oktobatunatiki






Social Plugin