Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NDULE RASMI KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM KWA NAFASI YA DIWANI KATA YA VING'AWE JIMBO LA MPWAPWA



Na Barnabas Kisengi, Dodoma

Shangwe, nderemo na vifijo vilitawala leo katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ving'awe Jimbo la Mpwapwa baada ya Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Emanuel Ndule kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Wanachama wa CCM, wananchi wa kata ya ving"awe walijitokeza kwa wingi kumsindikiza Mhe. Emanuel Ndule katika hatua hiyo muhimu ya kisiasa. Tukio hilo limeonyesha mshikamano mkubwa wa wana CCM wa kata hiyo, ishara ya umoja kuelekea ushindi wa chama hicho katika uchaguzi ujao.

Akizungumza katika ofisi ya Mtendaji wa Kata mara baada ya Mgombea kuchukua fomu Mhe Diwani mtarajiwa wa CCM Emanuel Ndule amesema kuwa chama hicho kina utaratibu wa kidemokrasia wa kupitia mchakato wa ndani na kuteua mgombea mmoja wa nafasi ya Udiwani, ambaye sasa ni Mimi Mhe. Emanuel Ndule.

“Sisi kama chama, tukimaliza uchaguzi wa ndani, tunavunja makundi yote yaliyokuwepo na sasa tunakuwa kitu kimoja – chama kimoja na kundi moja la wana CCM – kwa lengo la kuhakikisha wagombea wetu walioteuliwa wanashinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu,” alieleza Ndule

Ndule amesema hata Mimi nilikuwa na kundi langu kama waliyokuwa wenzangu tuliotia nia nao sote tulikuwa na makundi yetu kama sisi tuliotia nia tulikuwa 11 na tunaendelea na michakato ya vikao ndani ya chama tukarudi watia nia 3 Dickisoni Mahui ambaye alikuwa anatetea nafasi yake, mwingine alikuwa chazzy Magaya na Mimi Emanuel Ndule na baada ya mchakato wa kura za maoni ya ndani ya chama na vikao vyetu vya ndani ya chama ndio vilinithibitisha kuwa Mgombea halali kupitia chama changu cha Mapinduzi kwa nafasi ya Diwani wa kata ya VING'AWE.

Akikabidhi fomu za kugombea nafasi ya UDIWANI kwa Mhe. Emanuel Ndule, Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata ya Ving"awe Bi. Kogla Mgela alimwelekeza Mgombea kuzisoma kwa umakini na kuzijaza kikamilifu kama inavyoelekezwa kabla ya kuzirejesha kwa wakati uliopangwa na tume huru ya uchaguzi.

Baada ya kupokea fomu, Mhe.Emanul Ndule alitoa shukrani kwa chama chake kwa imani waliyoionyesha kwake, pamoja na Tume Huru ya Uchaguzi kwa kurahisisha mchakato wa kuchukua fomu hiyo.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu, chama changu, pamoja na familia yangu na wana Ving"awe wote kwa kuniunga mkono. Nashukuru tume kwa ufanisi wa mchakato huu – hakuna changamoto yoyote nimekutana nayo,” alisema Ndule

Akiwahutubia wananchi na wanachama waliomsindikiza, ndule aliwaahidi kuendeleza miradi yote iliyoanzishwa na aliyekuwa Diwani mstaafu Dickinson Mahui na kuhakikisha inakamilika kwa wakati. Alitaja mifano katika sekta ya Elimu na afya.

Mhe ndule alitaja vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, hasa katika Mtaa yake yote, kuboresha Elimu,afya, huduma ya soko la kata ya Ving"awe, michezo kwa vijana tena kwakuwa naye ni Diwani kijana.

Vipaumbele vingine ni ,kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama katika mitaa yote na kuhakikisha mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa na kusimamia na kuhamasisha shughuli za maendeleo kwa ushirikiano na wananchi wote wa kata hiyo.

Amehitimisha kwa kuahidi kuwa uongozi wake utakuwa wa ushirikiano, uwazi na kushirikisha wananchi wote bila ubaguzi, ili kwa pamoja kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi unatekelezwa vizuri kuijenga Ving"awe ya matarajio mpya yenye maendeleo endelevu.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com