Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MPINA AWASHA MOTO WA DEMOKRASIA, AWATAKA VIJANA KUCHUKUA NAFASI



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Mgombea urais wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema ataanza rasmi kampeni ya kukusanya wadhamini kwa wito wa kizalendo unaowalenga vijana na mshikamano wa kitaifa. 

Aidha amesisitiza kuwa safari yake ya kuingia Ikulu inalenga kuunganisha Watanzania bila kujali tofauti za kisiasa wala dini.

Akiwa Jijini Dodoma leo Agosti 15, 2025, baada ya kuchukua fomu ya uteuzi wa mgombea kiti cha urais katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mpina ameongozana na mgombea mwenza , Fatma Abdulhabib Fejej na kueleza kuwa mchakato wa kutafuta wadhamini utaanza Mwandoya, kijiji alichozaliwa mkoani Simiyu, kisha kuendelea kote nchini.

“Safari hii si ya chama pekee, bali ya taifa,tunataka vijana wajitokeze kwa wingi, wajue kwamba wanashiriki kuandika historia mpya ya Tanzania,” amesema.

Mpina ameweka wazi kuwa dhamira yake ni kuhakikisha kila hatua ya mchakato huu inaleta mshikamano na mshikikano wa jamii, huku akiahidi kutangaza ajenda kuu za ACT Wazalendo mara tu uungwaji mkono wa wadhamini utakapokamilika.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com