Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Juma Khamis Faki (kushoto) wakionesha begi la fomu za uteuzi walilokabidhiwa na Tume.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akielekezwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndg Ramadhani Kailima namna ya kusaini kitabu.

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akisaini kitabu.Mgombea Mwenza, Mhe. Juma Khamis Faki akisaini kitabu.
Wajumbe wa Tume wakiwa katika utoaji fomu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza wakati wa utoaji fomu za uteuzi kwa wagombea wa Chama cha UDP.
Wagombea wa Chama cha UDP wakiwa ukumbini.
Baadhi ya wanachama wa UDP wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu.
Baadhi ya wanachama wa UDP wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu.
Baadhi ya wanachama wa UDP wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu.

Baadhi ya wanachama wa UDP wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu.
Mgombea wa UDP akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu.
Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Mgombea Urais wa Chama cha United Democratic Party (UDP), Saum Hussen Rashid, pamoja na mgombea mwenza Juma Hamis Faki, wamechukua rasmi fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama hicho.
Fomu hizo zimekabidhiwa leo Agosti 14, 2025 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, katika hafla iliyofanyika makao makuu ya tume hiyo jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Saum ameishukuru INEC kwa mapokezi na utaratibu mzuri wa utoaji fomu, akibainisha kuwa chama chake kinaamini huu ni mwanzo wa uchaguzi huru na wa haki.
“Kama chama tumejipanga kuondoa changamoto zote kwenye jamii na kuwainua wananchi wanyonge, tunaamini Watanzania wanaweza kufanya maamuzi sahihi,” amesema.
Ameongeza kuwa vipaumbele vya UDP vinahusisha kuendelea kudumisha amani na utulivu vilivyoasisiwa na waasisi wa taifa, kutumia njia za amani kutatua migogoro, kuondoa ukatili wa kijinsia, na kuhakikisha rasilimali zote zinawanufaisha wananchi wote bila ubaguzi.
Kwa mujibu wa ratiba ya INEC, uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais unatarajiwa kufanyika Agosti 27, 2025.

Social Plugin