Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHEREHANI ACHUKUA FOMU YA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA USHETU KUPITIA CCM



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ushetu, Wilaya ya Kahama, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Emmanuel Cherehani , leo Agosti 24, 2025, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.


Cherehani ambaye aliteuliwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa kupeperusha bendera ya chama hicho amepokelewa na kukabidhiwa fomu hiyo na Afisa Uchaguzi katika Jimbo hilo Charles Mburu.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, Cherehani amekishukuru Chama chake na wananchi kwa imani waliompa huku akisisitiza mshikamano ndani ya chama na kuondoa makundi ya makambi ili kujenga Ushetu yenye mshikamano na maendeleo kwa manufaa ya wananchi wote.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com