Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wametakiwa kuzingatia ulinzi na usalama wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi haswa katika kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu.Akifungua mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Red Cross na mkufunzi wa Ulinzi na Usalama Amina Saidi ambaye ni mwandishi wa Habari baada ya kujengewa uwezo na umoja wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)kwa kushirikiana( IMS)Kisha kutakiwa kuwajengea uwezo waandishi wenzao ili wawe salama katika maeneo yao ya kazi.
Amesema kuwa Ulinzi na Usalama wa mwandishi wa Habari huanza na yeye mwenyewe hivyo ni lazima kutambua mazingira anayofanyia kazi na watu anaofanya nao kazi ili kujihakikishia Ulinzi na Usalama anapokuwa katika majukumu yake ya kazi.
Aidha amewataka waandishi wa Habari kuwa na desturi ya kujali usalama wao kwanza kwa kufuata Sheria na kanuni ili kujiepusha na changamoto zitakazojitokeza .
Kwa upande wake mshiriki wa Semina hiyo Rebecca Duwe amesema mafunzo hayo yamemuongezea uwelewa mkubwa wa kujua mipaka yake kama mwandishi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kazi haswa tunapoelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa International Media Support (IMS)Union of Tanzania Press Clubs (UTPC) na JamiiAfrica, ambapo miongoni mwa miradi hiyo ni kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama wa mwandishi wa Habari,Digital Safety,training and Tackling online ,Gender_ Based Violence for women Journalist.







Social Plugin