Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AHMED ALLY SALUM : ASANTENI KWA KUNIAMINI, KUENDELEA KUWATUMIKIA SOLWA

 


Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Ahmed Ally Salum, ameushukuru uongozi wa chama hicho na wanachama wake kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kuwatumikia, akisema imani hiyo ni kielelezo cha mshikamano  ndani ya CCM.



Katika ujumbe wake wa shukrani, Ahmed Salum amesema safari ya mafanikio ndani ya chama si ya mtu mmoja, bali ni matokeo ya mshirikiano wa pamoja, mshauri na dua za wanachama na viongozi.

“Naomba niwahakikishie kuwa nitazidi kusimama imara kwa uadilifu, uwajibikaji na bidii katika kuhakikisha lengo kuu la chama chetu linafanikishwa kuwatumikia wananchi, kuimarisha maendeleo na kuhakikisha CCM inaendelea kushinda kwa kishindo,” amesema Ahmed.

Amesisitiza kuwa ushirikiano huo ndiyo unaoimarisha misingi ya chama na kuleta mshikikano wa kweli wa kisiasa, huku akiwataka wanachama waendelee kushirikiana bega kwa bega katika kuelekea ushindi wa chaguzi zijazo.

Aidha, amemuomba Mwenyezi Mungu aibariki CCM na kuendelea kuilinda Tanzania, akihitimisha kwa kaulimbiu ya chama chake:“Kazi na Utu, Tunasonga Mbele!”


Soma ujumbe wote hapa

  SHUKRANI

Kwa unyenyekevu mkubwa na kwa moyo wa dhati, napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa Chama Changu Cha Mapinduzi (CCM), uongozi wake wote, pamoja na wanachama wenzangu kwa kuendelea kuniamini na kunipa heshima ya kuwatumikia. Imani yenu kwangu ni ishara kubwa ya mshikamano, mshikikano na upendo tulio nao ndani ya chama chetu.

Ninatambua kwa kina kuwa safari ya mafanikio si ya mtu mmoja bali ni matunda ya mshirikiano wa pamoja. Upendo, mshikamano, mshauri na dua zenu njema ndizo nguzo kuu zinazoniimarisha kila siku. Bila ushirikiano wenu, mafanikio haya tusingeyafikia.

Naomba niwahakikishie kuwa nitazidi kusimama imara kwa uadilifu, uwajibikaji na bidii katika kuhakikisha lengo kuu la chama chetu linafanikishwa—kuwatumikia wananchi, kuimarisha maendeleo na kuhakikisha CCM inaendelea kushinda kwa kishindo.

Namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kutujaalia afya, uzima, hekima na mshikamani ili kwa pamoja tuzidi kusonga mbele, tukijipanga kwa mshikamano na mshauri kwa ushindi mnono wa chama chetu katika chaguzi zijazo.

Kwa dhati kabisa, nawashukuru wote kwa kuniunga mkono, kwa maneno ya faraja, kwa dua, na kwa mshirikiano wenu usiokuwa na kifani. Ni imani yangu kubwa kuwa mshirikiano huu utaendelea kudumu na kuimarika zaidi.

📍Mungu aendelee kuibariki CCM.

Mungu aibariki Tanzania.

_KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE!_✅✅

      Mwisho

Mhe. Ahmed Salum

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com